Na Erick Evarist, Ijumaa
Madai ya Kumuita Mama Kanumba Kubwa Jinga…
KITENDO
cha muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kudaiwa kutoa
maneno yenye kuonesha sawa na kumtusi mama mzazi wa marehemu Steven
Kanumba, Flora Mtegoa, baadhi ya watu wamesema kuna dalili za msichana
huyo kuitafuta laana.
Hivi
karibuni, mama Kanumba aliliambia gazeti moja nchini (siyo ya Global
Publishers) kuwa tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mwanaye imebadilika
sana na kukosa maadili, kiasi cha kumuita yeye kuwa ni kubwa jinga.
“Hata
kama siyo mama yake mzazi, lakini umri tu unatosha kumuonesha kuwa
anahitaji kumheshimu, huwezi kumuita mtu aliyekuzidi kubwa jinga,
vinginevyo ni utovu mkubwa wa nidhamu na kwa mujibu wa mila na desturi
za Watanzania, huku ni kama kutafuta laana, mama Kanumba ni kama mzazi
wake,” alisema msomaji mmoja wa gazeti hili, aliyejitambulisha kwa jina
la Tabia Doffa wa Kimara.
Msomaji
mwingine aliyepiga simu chumba cha habari kutoka Tanga, aliyelitaja
jina lake kama Aesha, alisema kinachoonekana umaarufu umempa upofu,
kiasi cha kushindwa kuwaheshimu watu wanaomzidi umri, tena mtu ambaye
angeweza kuwa mama mkwe wake, ikizingatiwa kuwa Lulu alikuwa mpenzi wa
Kanumba.
“Huyu
mtoto umaarufu umempoteza, huwezi kutoa maneno kama hayo kumwambia mtu
ambaye angeweza kuwa mkweo, hivi kama Kanumba angekuwa hai angeweza
kumwambia namna hiyo? Hili ni tatizo la malezi, mambo mengine ya ustaa
ni ulimbukeni tu, laana inamnyemelea huyu,” alisema Aesha.
Akizungumzia
suala hilo, mama Kanumba alisema anasikitishwa sana na tabia ya
msichana huyo, kwani kikubwa ambacho angefarijika kupata toka kwake ni
heshima tu na wala si kingine chochote.
“Sielewi
jambo gani limemtokea huyo binti mpaka kufikia hatua ya kuniita hivyo,
lakini yote namwachia Mungu maana anajua anachokifanya,” alisema mama
huyo huku akionekana kulengwa na machozi.
Kwa
upande wake, alipoulizwa kuhusu kutoa kauli nzito kwa mama huyo, Lulu
alisema hapendi kumzungumzia chochote kwani siyo staili yake kuzungumzia
mambo ya wengine katika vyombo vya habari.
“Kama
yeye amesema hivyo kwenye vyombo vya habari ni staili yake, mimi staili
yangu ni ya kukaa kimya, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mama,” alisema
Lulu.
0 comments:
Post a Comment