Sunday, April 3, 2016



Barnana Zorro na Mpoto

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto pamoja na Banana Zorro wamepata shavu la kuandaa wimbo wa kuhamasisha jamii kuhusu usafi kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Mpoto Mpoto, instagram aliandika:
Saa saba usiku wakati wengine wamelala.sisi tupo macho studio, kujenga historia Mpya ya Dar es salaam na Mh Mkuu wa mkoa.
Baada ya kauli hiyo, Bongo5 ilimtafuta na kuzungumza na Mpoto kuhusu kazi hiyo.
“Yeah kuna kazi tunaandaa,” alisema Mpoto. “Ni wimbo ambao utakuwa unatumika katika kampeni za safi wa mazingira katika mkoa wa Dar es salaam”. alifafanua zaidi Mpoto.
Wimbo huo unaandaliwa na mtayarishaji mkongwe wa muziki, Allan Mapigo.

0 comments:

Post a Comment