Saturday, April 9, 2016











MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa

Tanzania, Mbwana Ally Samatta

ametokea benchi na kuifungia timu

yake, KRC Genk katika ushindi wa

4-0 dhidi ya KV Oostende kwenye

mchezo wa Ligi Ku ya Ubelgiji

usiku huu.


Katika mchezo huo uliofanyika

Uwanja wa Cristal Arena, mjini Genk,

Nahodha wa Tanzania, Samatta

alifunga bao hilo dakika ya 77, ikiwa

ni dakika moja tu baada ya kuingia

kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.

Mabao mengine ya Genk

yamefungwa na Pozuelo dakika ya

12, T. Buffel dakika ya 21 na N.

Kebano dakika ya 85.


Hilo linakuwa bao la tatu kwa

Samatta katika mechi nane

alizocheza tangu ajiunge na Genk

Januari mwaka huu akitokea TP

Mazembe ya DRC.


Kabla ya kufunga katika ushindi wa

4-1 dhidi ya KV Oostende, Samatta

pia alifunga katika ushindi wa 3-2

baada ya kuingia dakika 15 za

mwisho dhidi ya Club Brugge.


Mechi nyingine alizocheza Samatta

tangu atue Genk, zote akitokea

benchi dakika za mwishoni ni dhidi

ya Standard Liege (Genk)

wakifungwa 2-1, dhidi ya Lokeren

wakitoa sare ya 0-0, dhidi ya

Waasland-Beveren wakishinda 6-1

na dhidi ya Mouscron-Peruwelz

wakishinda 1-0 pia ugenini na dhidi

ya Anderlecht wakifungwa 1-0.































MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa

Tanzania, Mbwana Ally Samatta

ametokea benchi na kuifungia timu

yake, KRC Genk katika ushindi wa

4-0 dhidi ya KV Oostende kwenye

mchezo wa Ligi Ku ya Ubelgiji

usiku huu.


Katika mchezo huo uliofanyika

Uwanja wa Cristal Arena, mjini Genk,

Nahodha wa Tanzania, Samatta

alifunga bao hilo dakika ya 77, ikiwa

ni dakika moja tu baada ya kuingia

kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.

Mabao mengine ya Genk

yamefungwa na Pozuelo dakika ya

12, T. Buffel dakika ya 21 na N.

Kebano dakika ya 85.


Hilo linakuwa bao la tatu kwa

Samatta katika mechi nane

alizocheza tangu ajiunge na Genk

Januari mwaka huu akitokea TP

Mazembe ya DRC.


Kabla ya kufunga katika ushindi wa

4-1 dhidi ya KV Oostende, Samatta

pia alifunga katika ushindi wa 3-2

baada ya kuingia dakika 15 za

mwisho dhidi ya Club Brugge.


Mechi nyingine alizocheza Samatta

tangu atue Genk, zote akitokea

benchi dakika za mwishoni ni dhidi

ya Standard Liege (Genk)

wakifungwa 2-1, dhidi ya Lokeren

wakitoa sare ya 0-0, dhidi ya

Waasland-Beveren wakishinda 6-1

na dhidi ya Mouscron-Peruwelz

wakishinda 1-0 pia ugenini na dhidi

ya Anderlecht wakifungwa 1-0.













on

0 comments:

Post a Comment