Friday, April 15, 2016

Tuddy Thomas
Mtayarishaji wa muziki nchini, Tussy Thomas amesema kuwa nyimbo ya Mdogo Mdogo ya Diamond Platinumz ndiyo ambayo ilimfungulia milango ya kupata dili za kuwatengenezea midundo wasanii wakubwa Afrika.

Akizungumza katika kipindi cha XXL kinachorushwa kupitia Redio Clouds Fm, Tuddy Thomas alisema amekuwa akipokea ofa kutoka kwa wasanii mbalimbali walio na majina Afrika wakihitaji kufanya nae kazi.
“Mungu anasaidia nimepata kazi kutoka kwa wasanii wakubwa Afrika kama Iyanya na Wizkid … Wizkid tuliwasiliana na nilishamtumia mdundo nasubiri nione itakuwaje,” alisema Tuddy Thomas.

0 comments:

Post a Comment