Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiana Lubuva akisalimiana na Catographia Bwana Brian Mhonda toka Tume ya Uchaguzi Zimbabwe walipofika ofisi kwake kusalimiana naye. Katikati toka kushoto ni Kaimu Mkuu wa sehemu ya Catographia toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Adolph Kinyero na Afisa Uchaguzi wa Wilaya Toka Tume ya Uchaguzi Zimbabwe Collins Chamunorwa Muchenjekwa
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Christina Njovu-NEC
Ujumbe kutoka Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) umekuja kujifunza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jinsi ilivyoendesha zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura kwa kutumia Mfumo wa Biometrick Voter Registration (BVR) kwa kuwa Tanzania ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuandikisha wapiga Kura wengi kwa kutumia technologia hiyo mpya.
Wakizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaafu Damian Lubuva ujumbe huo wa watu wawili Brian Mhonda na Collins C. Muchenjekwa toka Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe wameeleza kuwa; Zimbabwe ipo katika maandalizi ya kuandikisha Wapiga Kura.
Ujumbe huo umeeleza kuwa; Zimbabwe imeichagua Tanzania nchi ambayo imefanya uandikishaji wa Wapiga Kura hivi karibuni na kufanikiwa kuandikisha watu wengi kwa muda mfupi kwa kutumia mfumo wa BVR.
“Tupo katika maandalizi ya kuandikisha Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) mfumo ambao Tume yetu imeuchagua kutokana na kukua kwa Technolojia duniani” Mfumo huu kwa Zimbabwe utatumika kwa mara ya kwanza” alisema bwana Muchenjekwa.
Wakiwa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ujumbe huo ulijifunza namna Elimu ya Mpiga Kura ilivyotolewa kiasi cha kuwafikia watu wengi ambao walijitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Katika Ziara hiyo ya mafunzo,wajumbe hao walihitaji kujifunza zaidi njia na mbinu mbalimbali za kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili iweze kuwafikia wananchi wengi ili wajitokeze kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Sambamba na hilo walijifunza namna ya kusoma ramani ya Majimbo ya Uchaguzi na Jinsi gani Tume ilifanya manunuzi ya vifaa vya Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Ujumbe huo ulijikita zaidi katika kujifunza jinsi Biometrick Voter Registration (BVR) namna inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza kwa kuchagua kuja kujifunza nchini Tanzania kwani kitendo hicho kinaipa heshima NEC na Tanzania kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment