Ni
takribani mwezi mmoja sasa tangu Diamond na Kanye West walipokutana
kwenye uwanja wa ndege, Los Angeles nchini Marekani na kupiga picha ya
pamoja.
Hivi karibuni maneno yameanza kuzuka tena mitaani kuhusu
picha hiyo waliyopiga Diamond na Yeezy. Watu wanazungumza kwanini
alinuna kwenye ile picha?
Akiongea kwenye stori tatu ya Planet Bongo,
inayoruka kupitia EA Radio, Diamond amesema, “Nafikiria ni attitude ya
Kanye ndivyo alivyo.”
“Ananuna hata akipiga picha na mkewe na mkwe wake, nafikiria nilipata bahati kwenye ile picha yangu kidogo alifurahi. Kuhusu collabo chochote kinaweza kutokea tumuombe Mungu. Naposema nataka muziki wetu upenye Marekani ni kujaribu kwenda kupambana na wale manguli wao ili tuone itakuwaje,” aliongeza.

0 comments:
Post a Comment