Sunday, April 24, 2016


Uzinduzi wa video ya NdiNdiNdi ambao umefanyika katika kituo cha EATV kwenye kipindi cha 'Friday Night Live' FNL umewafanya mashabiki wa Bongo Flava na wapenzi wa Lady JayDee kushughudia mwanzo mwisho uzinduzi huo.

Katika maeneo mengi ya starehe na majumbani watu walihamishia macho yao katika kituo cha EATV kujionea namna mwanadada Lady JayDee alivyofanya vyema katika video hiyo.
Aidha katika screen ambayo ilikuwa live kuonyesha namna watazamaji wanavyouliza maswali kwenye mitandao ya kijamii na kumpongeza msanii huyo ilionekana ikiingiza ujumbe kuanzia mwanzo wa kipindi hadi mwisho wa kipindi hicho.
Hata hivyo msanii Lady JayDee amewaomba mashabiki wake waendelee kumuunga mkono katika kazi zake na kwamba ataendelea kuwaletea vitu vikali zaidi.

0 comments:

Post a Comment