Posted by Williammalecela.com on Saturday, May 07, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akihutubia wadau wa michezo na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa mashindano ua UMISSETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola.Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo mbalimbali na burudani za kila aina zilikuwepo.
Meneja wa Kiwanda cha Coca Cola tawi la Mbeya, Gary pay (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ndani ya Uwanja wa Sokoine Mbeya kwenye uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla akigagua moja ya timu wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo kwenye uwanja wa mpira wa Sokoine.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi hyuo wa mashindano ya UMISSETA wakiwa katika uwanja wa Sokoine.
Burudani za muziki pia zilikuwepo kama kinavyoonekana kikundi hiki kikitumuiza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment