
Rais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji.
Kupitia akaunti yake ya Twitter mshauri wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe amethibitishwa kuwa rais huyo wa zamani wa nchi ya Burundi amefariki dunia akiwa nchini Ubelgiji.
Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi na aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu wake Meja Pierre Buyoya Septemba 1987.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment