Jeshi la wanahewa la Afrika Kusini
limesema duma wawili, ambao hufugwa kwenye kambi ya jeshi hilo ili
kufukuza wanyama wengine njia ya kutumiwa na ndege kupaa, wamemshambulia
afisa wa jeshi.
Msemaji wa jeshi hilo Marthie Visser amesema
kupitia taarifa kwamba duma hao waliingia eneo ambalo ndege huegeshwa
katika eneo la Makhado.
Mwanajeshi aliyekuwa kwenye zamu aliwaona na kujaribu kuwapiga picha na hapo ndipo wakamshambulia.
Mwanajeshi huyo hakujeruhiwa vibaya na ameachiliwa kutoka hospitalini.
Wanyama hao hawatafukuzwa katika kambi hiyo.
Bi
Visser alisema kambi hiyo, iliyo kaskazini mwa Afrika Kusini,
imezingirwa na mbuga za wanyama na duma hao husaidia kudhibiti ongezeko
la wanyama mwitu.

0 comments:
Post a Comment