Friday, May 6, 2016

12748343_1005700972855425_1813264444_n
Janet Jackson ni mjamzito, akiwa na umri wa miaka 49. Atakuwa mtoto wao wa kwanza na mumewe, Wissam Al Mana.



Habari hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo kutangaza kusitisha ziara yake ya Unbreakable kwa kile alichoeleza kama kupanga familia yao.
Alisema kuwa alilazimika kufanya hivyo kutokana na maagizo ya daktari.

Chanzo kimoja kiliiambia E! News Jumatano hii kuwa ujauzito wake upo kwenye trimester ya pili na kwamba yeye na mume wake Al Mana wamekuwa wakifanya kazi na mtaalam wa masuala ya ushkaji mimba kwa muda.
Ni nadra sana kwa mwanamke wa umri wake kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. Wengi wanaoshika hutumia njia ya IVF, kwa kutumia mayai yao wenyewe waliyoyagandisha wakati wa miaka yao waliyokuwa na uwezo wa kuzaa au kupewa yai la wanawake wadogo.
Janet na Al Mana, bilionea wa Qatar mwenye miaka 41 walifunga ndoa mwaka 2012.

0 comments:

Post a Comment