Mmiliki wa lebel ya muziki ya PKP ‘‘Poz Kwa Poz Entertainment’ Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa May 5 2016 atamtambulisha ramsi msanii mpya ‘Nedy Music’ kupitia lebel hio.
PKP imeshatayarisha video kali ya Nedy Music iliyofanywa na Justin Campos wa Afrika Kusini. Wimbo wa Nedy umeitwa ‘Usiende Mbali’.
Gazeti la Mwanaspoti, limeongea na Mubenga ambaye amethibitisha taarifa hizi kwa kusema “Tunatarajia kuachia video mpya ambayo kwa mara ya kwanza tangu tumemchukua tunatoa kazi yake, wimbo unaitwa ‘Usiende Mbali’ na audio tumefanyia pale kwa Nahreel Industry na video tumefanyia Afrika Kusini kwa Director Justin Campos,”
Ommy Dimpoz alitangaza kumtoa msanii kwenye lebel yake ya PKP miaka miwili iliyopita wakati wanaitambulisha lebel hii.
Pata Stori Kirahisi Zaidi,FahamuTv.Com Ipo Instagram>INSTAGRAM
0 comments:
Post a Comment