Msanii M 2The P ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa msanii Albert Mangwea, amesema hadi leo anahisi kuna mtu aliyehusika na kifo cha Ngwea, na kumfanya ashindwe kuamini ni ajali ya kawaida.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East AfricaRadio, M2The P amesema kitendo cha kuibiwa vitu vyao vyote ndio kilichompa wasi wasi.
"Unajua ile siku tuli-party sana, tumepiga bata lakini kilichonishtua, ni sawa tukio lilikuwa kama ilivyoonekana ila kilichonishangaza ni baada ya kurudi ghetto tukakuta vitu vyote vimeibiwa, kitu kilichonishtua, ina maana ilikuwa ni kama walitu-target kabisa," alisema M 2TheP.
Pia msanii huyo ambaye naye siku ya tuko hakuwa katika hali nzuri baada ya kupoteza fahamu, amesema kulingana na hali hiyo, anaunga mkono kauli ya mama mzazi wa Ngwea Bi. Denisia Constantino, kwamba huenda kuna watu walishiriki kusababisha kifo cha Ngwea.
0 comments:
Post a Comment