M toto wa marehemu Anathe, Allan Kimario (aliyelala).
Majonzi
na huzuni vimetawala kwenye tukio la kuagwa kwa mwili wa mdogo wa
Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa risasi mwaka 2013, Anathe Simon
Msuya ambaye yeye aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kigamboni
jijini Dar, Mei 25 mwaka huu.
Mamia
ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala
jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa
akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia kuangua vilio walipokuwa
wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za
mwisho.
Mtoto
wa Anathe aliyetajwa kwa jina la Alan Kimario (4) alionekana
akilazimishwa kwenda kuuaga mwili wa mama yake kwani alikuwa akitaka
aachwe aendelee na michezo yake kutokana na ukweli kwamba, alikuwa hajui
hata kinachoendelea.
Mwili
wa marehemu Anathe umesafirishwa kwenda Mererani jijini Arusha kwa
ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho (Jumanne).
Mungu ailaze roho ya marehemu Anathe mahali pema peponi. Amin!
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
0 comments:
Post a Comment