Tuesday, May 10, 2016

13150962_1101873753209256_1518965762_n
Unakumbuka kipindi Kanye West na Kim Kardashian wameanzisha uhusiano wao? Watu waliwapa siku chache tu wakiamini kuwa penzi lao haliwezi kudumu.

Leo hii ni wanandoa, wana watoto wawili na penzi lao bado lipo imara. Ndivyo ilivyoonekana kwa Barakah Da Prince na Naj pia. Ni kwasababu katika kipindi kifupi tangu aanze kuvuma, Barakah alihusishwa kuwa na uhusiano na warembo A-List wakiwemo Linah, Meninah, Masogange na hadi Nisha.
13151347_177319679330322_462422885_n
Hivyo wengi walivyosikia kuwa muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ kahamishia mapenzi kwa Naj, walijua napo anapita tu. Pia ni kutokana na mahusiano mengi ya mastaa hayadumu. Guess Barakah anaweza kutuprove wrong kwasababu kuna kila dalili kuwa penzi lao limezidi kushika mizizi zaidi na hawataki tena kulificha.
12965704_1124390794248358_1010721261_n
Swali ni je wataendelea kuwa pamoja kwa miaka mingi ijayo?

0 comments:

Post a Comment