Leo tarehe 20 May 2016 saa saba kamili mchana aliyekuwa katibu mkuu wa UVCCM Mh Sixtus Mapunda ambae kwa sasa Ni Mbunge wa Mbinga Mjini amekabidhi rasmi ofisi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM ndugu Shaka Hamdu Shaka ambae alikiwa naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar.
Kutokana na kubanwa na Majukumu ya Ubunge na kuongeza ufanisi wa ofisi ya Vijana Mh Sixtus Mapunda amekabidhi ofisi rasmi Ili kutoa nafasi zaidi kwa Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Shaka Kusimamia ofisi vizuri zaidi.
Umoja wa vijana unatoa Pongezi na shukurani kwa Mh Sixtus Kwa utumishi wake wote ndani ya UVCCM na tunamtakia kila la kheri Katika utumishi wake mpya kama mbunge wa mkoa wa Ruvuma.
Aliitumikia CCM na UVCCM kwa dhati na muda mrefu hadi sasa amekuwa Mbunge wa CCM ni imani yetu kuwa ataendelea kuwa karibu wakati wote kwa Maslahi ya CCM
Tunawaomba Vijana wa CCM na Watanzania wote nchi nzima kumpa ushirikiano wa kutosha Kaimu katibu Mkuu ndugu Shaka Hamdu ili kuiendeleza jumuiya yetu Mbele zaidi kwa Maslahi ya Chama na nchi yetu.
Imetolewa na :
ABUBAKAR D. ASENGA
KAIMU MKUU WA IDARA Hamasa, Sera,utafiti na mawasiliano
UVCCM MAKAO MAKUU
ABUBAKAR D. ASENGA
KAIMU MKUU WA IDARA Hamasa, Sera,utafiti na mawasiliano
UVCCM MAKAO MAKUU
0 comments:
Post a Comment