Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
MREMBO wa nguvu, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
amefunguka kuwa katika orodha ya wasanii wa Bongo Fleva anaowakubali
kwa sasa Bongo, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ ameuteka vilivyo moyo
wake.
Kidoti amefunguka hayo juzikati
alipokuwa akipiga stori na mwanahabari wetu ambapo alipoulizwa kuhusu
msanii wa Bongo Fleva anayemkubali zaidi, Jokate alisema anamkubali
kinoma Baraka Da Prince.
“Yeah! Namkubali sana Baraka, ni mtu
ambaye anafanya vizuri kwa kweli ananikosha. Mwingine ni huyu Raymond,
naye nampenda,” alisema Jokate, mwanamitindo, mwigizaji na msanii wa
Bongo Fleva.

0 comments:
Post a Comment