Mwenyewe alipozungumza na Ijumaa Wikienda alisema kuwa, hajali watu wanavyomnanga kwa sababu yupo kimasilahi zaidi kwani amelipwa mkwanja mrefu ambao unakidhi mahitaji yake na anachojua yeye hajaonesha maungo yake bali anafanya matangazo ya nguo aliyoionesha.
“Dah! Najua nimetukanwa sana lakini watambue kuwa mimi ni Balozi wa EBM, kampuni ya nguo, wamenilipa mkwanja mrefu na kila nguo inayotua kwenye mwili wangu ni matangazo sasa siwezi kuwajali binadamu zaidi nikaacha masilahi, kikubwa sivunji sheria,” alisema.
0 comments:
Post a Comment