Video Queen na muigizaji wa filamu anayekuja juu kwa sasa Bongo, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ juzikati alizua timbwili kwenye fumanizi mitaa ya nyumbani kwao, Tandale jijini Dar lililomhusisha shemeji yake, Ijumaa inakuhabarisha.
Mapaparazi wetu walienda nyumbani kwa video queen huyo kwa ajili ya
mahojiano ya kawaida na mastaa, lakini wakiwa wameshakaribishwa na
kuanza maongezi, ghafla aliingia mdada mmoja na kumchukua staa huyo na
kuingia naye chumbani kwake. Muda mfupi baadaye walitoka na Lulu Diva
aliwaomba radhi waandishi wetu akiaga kuwa ‘anamtoa’ nje mgeni huyo
aliyesema ni dada yake.
Achelewa kurejea
Wakati mapaparazi wetu wakiwa wanamsubiri na kuona kabisa anachelewa
tofauti na ahadi yake, mara akaja jirani yake na kuwajuza kuwa mwenyeji
wao alikuwa mtaa wa pili, akiwa ‘amelianzisha’, kwani amemkuta shemeji
yake, yaani mwanaume anayeishi na dadake, akiwa ameingiza mchepuko
ndani.
“Jamani Lulu Diva huko anabwata balaa, watu wamemzunguka
nasikia amefumania, hamna habari nyie? Kama ndugu zake mpo nendeni
mkamsaidie,” alisema jirani huyo na kuondoka.
Mapaparazi eneo la tukio
Baada ya kusikia habari hizo, haraka mapaparazi wetu waliibuka mtaa wa
pili na kumkuta Lulu Diva akifoka, akimtaka shemeji yake aliyejifungia
ndani, atoke nje na mchepuko wake, lakini kwa mshangao wao, wawili hao
waliofumaniwa walitokea mlango wa upande wa pili na kutokomea
kusikojulikana.
Msikie sasa Lulu Diva
“Dah! Ni stori ndefu,
huyu aliyefumaniwa ni shemeji yangu, amenishangaza kuleta mwanamke ndani
wakati dada yangu kaenda kujifungua, leo karudi ndo tunamkuta shemeji
akipikiwa chai tena na mwanamke amevaa mtandio tu, imeniuma ndiyo maana
nimezua timbwili huyu mwanamke bado tutamtafuta tu,” alisema Lulu Diva.

0 comments:
Post a Comment