Friday, May 6, 2016

chk1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais,leo,[Picha na ikulu.]
chik2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na ikulu.]


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Japan hasa kwa kutambua hatua za nchi hiyo za kuendelea kuiiunga mkono Tanzania katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo.
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipofanya mazungumzo na Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe. Mathias Meinrad Chikawe
Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ikiwemo Zanzibar inajivunia uhusiano na ushirikiano mzuri pamoja na hatua za Japan za kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha miradi kadhaa hapa nchini.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Japan imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwamo miradi ya maji, umeme, kilimo, afya na miradi mengineyo.

0 comments:

Post a Comment