Zaidi ya viongozi mia moja wa mila kutoka kabila la maasai kwenye wilaya za watu wa jamii hiyo wamekusanyika wilayani Monduli mkoani Arusha kumsimika Kiongozi Mkuu wa mila wa koo ya Ilikisongo na kufanya ibada maalum ya kimila ya kumwombea Rais Magufuli na serikali yake waendelee kupambana na wafujaji wa mali ya umma.
Katika
tukio ilo lililohudhuriwa na viongozi wa mila kutoka wilaya za mikoa ya
Arusha, Manyara, Morogoro na kwingineko pamoja baadhi ya viongozi wa
kisiasa ambapo wengi wao ni wa jamii hiyo viongozi wa mila wamesema wapo
tayari kushirikiana na serikali katika kuwafichua watendaji wazembe na
wauza ardhi ya umma ili kuwaondoa watanzania kwenye dimbwi la
umasikini.
Kiongozi
aliyesimikwa kama mwenyekiti wa viongozi wa mila wa koo hiyo Kibori
Ngelipoi ,akizungumza huku akitafsiriwa kwakuwa hajui lugha ya kiswahili
amesema nafasi ya viongozi wa mila katika jamii ni kubwa naye
atahakikisha atatumia vizuri nafasi hiyo.
Baadhi
ya viongozi wa kisiasa waliohudhuria tukio hilo wamewaasa viongozi wa
mila kutochanganya siasa na mila kwa kuwa vitashusha ufanisi wao katika
kutatua masuala ya kijamii.
Chanzo-ITV
0 comments:
Post a Comment