Leo
i want to touch this very sensitive subject ya wanaodai kuwa inapokuja
kwenye diaspora huenda nina wivu na chuki na wanaoishi majuu kwa sababu
nilirudi, ha! ha! ha! kwa wale ambao hamjafika majuu naomba kusema
hivi:- mungu alinijalia sana confidence in myself na everything i do,
nilipofika majuu kwa mara ya kwanza nilikuta wabongo karibu wote pale
New York wanafanya kazi za kulinda na kutunza wazee na mataharia, siku
moja mbongo
mmoja alinipeleka kwenye kazi ya kutunza mataahira nilikaa
kama lisaa limoja tu sikurudi tena, nikaenda shule kutafuta leseni ya
cdl ya kuendesha malori makubwa sana ambayo hapa bongo hayapo, kazi
ambayo inalipa haswa nikahangaika mpaka nikapata ile leseni nikiwa
ninafanya kazi gas station mchana na usiku Kentucky Fried Chicken.
Nilipopata leseni nikaanza kuendesha malori America nzima. Wale wabongo
niliowakatalia zile kazi zao wakaanza kunizushia maneno kwamba ninauza
unga, ha! ha! ha! ha!,
Kabla ya kwenda New York nilishakuwa
baharia Belgium so Ulaya haikuwa kitu kigeni kwangu, ndio maana siku
moja nikaamua kurudi Bongo mwenyewe bila kulazimishwa na mtu. Cha kwanza
nilipofika tu bongo nikaanza kunenepa, why? Kwa sababu ni kwa mara ya
kwanza katika miaka 30 ya maisha yangu nimeweza ku-relax na maisha.
Majuu ni kufanya kazi tu na kulipia madeni, wazungu sio wajinga
wameitengeneza system yao to the point wewe unaenda kuchangia uchumi wao
tu hauwezi kuwa tajiri maana uwezekano haupo, wewe ni kazi tu, social
life hamna ni kazi tu kila ukikaa unawaza kazi, mabebez hamna, wachache
wabongo waliopo ni hasara tupu wengi wao hawajitambui. Kwenye uzungu
hawapo kwenye ubongo hawapo wapowapo tu ole wako uwaguse, i mean kila
kitu majuu ni perfect lakini gharama yake haikupi nafasi wewe kuwa na
pesa extra, ndio unagundua kwamba majuu sio kama ulivyotegemea maisha ni
mazuri lakini magumu sana kurudi bongo nako huwezi maana ni noma zaidi
so you are stuck, i was stuck too mpaka nilipoamua kwa hiari yangu
kurudi home.
Hapa sina deni kwa mara ya kwanza katika maisha
yangu, sidaiwi na mtu kila nilichonacho, kama ni gari ni langu,
apartment ni yangu, shamba na nyumba ni vyangu sidaiwi na mtu, nafanya
kazi ya kujiajiri, nakuja kazini saa ninayotaka, ninatoka saa
ninayotaka, kwa mara ya kwanza ninamiliki simu za usd $ 1000 a piece
majuu ningekuwa nayo ya kukopa na sikuwahi kuwanazo, bongo maisha baada
ya kazi hayana mfano, marafiki kila kona kule unakuwa huna marafiki,
bongo heshima kila kona majuu mweusi atakuheshimu nani? i mean kwenye
kujiajiri nikipiga deal moja ikaitika millions zinakuwa zangu sio
kulipia madeni, ninasafiri bongo na nje ya bongo anytime i want majuu
nisingeweza maana ni kazi tu all the times.
Sasa naomba kuuliza
jamani kweli niwaonee wivu na chuki waliobaki majuu kwa kisa gani?
nasema hivi majuu wanatuzidi bongo kwa one thing matibabu wao wakiumwa
kule ni rahisi sana kupona kuliko hizi hospitali zetu bongo, ni hilo tu
mengine hapana bongo kuna maisha asikudanganye mtu, again mungu
alinijalia moyo wa kujali yangu zaidi na sio ya wengine so kwa wale
mnaolia lia kwamba nawaonea wivu eti mko majuu ha! ha! ha! ha! please!!,
ninafanya biashara na wabongo wengi huko nje inapokuja kwenye kulipa ni
kivumbi na patashika lakini hapa bongo ni tofauti watu wanalipa mara
moja tena mpaka kwa dola za kimarekani, jamani kwa wale ambao hamjafika
huko majuu na unaweza kula milo mitatu bongo bila tatizo tulieni hapa
hapa jamani huko majuu kusikieni tu!!, ninamshukuru mungu kila siku kwa
kunipa akili ya kwenda majuu na pia ya kurudi home ontime kabla
sijachelewa, ndugu zangu huko rudini huku bongo maisha ni sawa ila tu
ujipange kabla ya kuja na muhimu kuliko yote soma shule kwanza, huku
bongo bila elimu utachekesha maana hela ukijanazo zitaisha kama huna
elimu. jamani samahani kwa maelezo marefu lakini i hope nimemsaidia
somebody out there!! - Le mutuz.

swadaktaa kaka. wengi wanateswa na aibu kuwa wataonekaje, na kutojua wapi waanzie watakaporui home.. TURUDIGE HOME TUJENGE MAISHA WAJAMENI......>>>>>
ReplyDelete