Uingizaji Holela wa Samaki toka nje Mkuu wa Mkoa wa Mbeya atinga mpakani Kasumulu
Mkuu wa Mkoa kwa mara nyingine ametembelea kituo cha Forodha cha Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi na kuongea na wafanyakazi wa Forodha na kuwaagiza kuwa waangalifu na ukaguzi wa Samaki toka nje kwakuwa zipo taarifa kuwa kuja Samaki wanaingizwa toka nchi mbalimbali ikiwemo China wanaingizwa Namibia wanapitishwa Zambia Hatimae Tunduma na kuingia Songwe Mbeya na mikoa mingine hivyo amewataka wafanyakazi wa kituo cha Kasumulu kukagua Mazao yote ya uvuvi kama uingiaji wake umezingatia taratibu zote na ni salama kwa Afya ya binadamu
Imedaiwa baadhi wa Samaki si wazuri kwa Afya ya binadamu na uingiaji wake usipodhibitiwa walaji wana hatari ya kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo Kansa





0 comments:
Post a Comment