Bi. Mwanahawa Ally wa Zanzibar Stars akiimba.
Sabaha Salum akionyesha mashabiki utamu wa sauti yake.
Khadija Kopa wa TOT akitoa burudani.
Mashabiki wakiselebuka katika midundo ya ala mbalimbali.
Khadija Yusuf (kushoto) akicheza mbele ya Sabaha Salum.
Ikbar wa All Stars akighani.
Mustafa Ramadhani wa Egyptian Taarab akifanya vitu vyake.
Abdul Misambano wa Babloom Taarab akiburudisha.
ONYESHO
la taarabu lililopewa jina la Usiku wa Kale ambalo limefanyika usiku wa
kuamkia leo katika ukumbi wa Dar Live Mbagala-Zakhem, lilikuwa la aina
yake ambapo mashabiki walifaidi kila sekunde ya tukio hilo.
Usiku
huo ulioshirikisha bendi za zamani za taarabu za Muungano, Babloom,
TOT, Egyptian Taarab, East Africa Melody, Zanzibar Stars, All Stars
ulikuwa wa burudani ya aina yake kutokana na nyimbo zilizokuwa zikiimbwa
kuwakumbusha ‘mbali’ mashabiki.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)
0 comments:
Post a Comment