Yasmin Eleby
Yasmin
Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake
atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho
kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa
mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa
hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya
harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Duru
zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika
makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni
wengine waalikwa.
Kwa
sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni
kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya
watu wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana
na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana
kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi
hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.
Aliposikia
kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga
kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.
"Eleby
alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia
ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema
harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya
kijamii.
Anasema
anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza
kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu
kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.

0 comments:
Post a Comment