Na Musa Mateja, RISASI MCHANGANYIKO
DAR
ES SALAAM: Katika hali ya kushangaza, staa wa Bongo Fleva, Baraka
Andrew ‘Baraka Da Prince’ amenaswa akimdhalilisha staa mwenzake,
Estalina Sanga ‘Linah’ kwa kumshika sehemu zake nyeti.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita katika Ufukwe wa Escape
One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuadhimisha miaka kumi
ya staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama’.
Paparazi
wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage,
kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye
kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.
“Mh!
Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini
haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye
sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.
Alipoulizwa
na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa
kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea
kwenye himaya yake ya zamani.
“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa
upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri
Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya
kuishia kucheka tu.
Linah
na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja
kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.
0 comments:
Post a Comment