Mahakama Kuu kanda ya Arusha imetengua Ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa
jimbo la
Longido Mhe.Onesmo Ole Nangole (CHADEMA) kufuatia kesi ya udanyanyifu wa matokeo iliyofunguliwa na mpinzani wake Bw.Stephen Ole Keruswa (CCM).
Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Sivangilwa Mwangesi amesema upande wa mlalamikaji umeweza kudhibitisha tuhuma za udanganyifu wa matokeo katika uchaguzi huo, uliofanyika October mwaka jana.
Katika kesi ya msingi mgombea wa CCM Ole Keruswa alidai mbele ya mahakama kuwa Ole Nangoro alikula njama na msimamizi wa uchaguzi huo Ndg.Felix Kimario ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido ili kufanya udanganyifu.
Ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha kuwa idadi ya kura katika karatasi za matokeo ilitofautiana na idadi ya kura alizotangaza Msimamizi wa uchaguzi Ndg.Kimario kwa kura 149.
Katika uchaguzi huo Onesmo Ole Nangole (CHADEMA) alipata kura 20,076 dhidi ya mpinzani wake Stephen Ole Keruswa (CCM) aliyepata kura 19,352. Tofauti ya kura 724, huku idadi ya kura zilizoharibika ikiwa 767.
Upande wa malalamikaji ulidai kuwa Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye ni mkurugenzi wa Wilaya hiyo Ndg.Felix Kimario alikula njama (Conspirancy) na Bw.Ole Nangole ili kuharibu kura nyingi (767) kumuwezesha Ole Nangole kupata ushindi mwembamba wa kura 724, maana katika hali ya kawaida haiwezekani idadi ya kura zilizoharibika izidi idadi ya kura za ushindi.

0 comments:
Post a Comment