Mwanamitindo Hamisa Hassani Mobeto, amekataa kuzungumzia mgogoro
unaodaiwa kuendelea kati yake na staa wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’
huku akionyesha kuchukizwa na jinsi mwanae anavyohusishwa katika mambo
yasiyo muhusu.
Hamisa Mobeto akiwa na mtoto wake
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mobeto amesema mtoto wake hana
hatia yoyote katika mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.
“Issue ya Lulu sijui na Majay siwezi zungumzia, kitu ambacho
kinaniumiza ni kumwingiza mwanangu kwenye haya mambo, na mtoto wangu
anakuwa anajumlishwa katika mambo ambayo hayamuhusu kabisa na hakupaswa
kuhusishwa,” alisema Mobeto. Kwa hiyo hakuna mzazi ambae angekubali
mwanaye azungumziwe hivyo au aongelewe kwenye mambo yasio mazuri,”
Aliongeza,” Ningekuwa sina mtoto wala nisinge umia lakini kwa sababu
kuna mtoto ambaye hana hatia wala hajui kinachoendelea, so sipendi hiki
kitu,”
Katika mitandao ya kijamii mashabiki wa Lulu na Hamisa wamekuwa
wakitupiana maneno huku chanzo kikidaiwa ni Majay, lakini Hamisa
alikataa kuzungumzia chochote kuhusu mpenzi wake huyo wa zamani.

0 comments:
Post a Comment