Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson.
Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO
HABARI
njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay
wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la
kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela.Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko,
Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi
mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka
Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa
atatumikia kifungo cha nje.
Nay
wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu
anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa
mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya
kumsaidia.
“Kulikuwa
kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo,
mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watamaliza.
“Hivi
ninavyoongea na wewe niko mbali na mjini lakini taarifa za Siwema
kutoka jela ninazo, kwa hiyo sina maelezo mengine zaidi ya hayo ila
namshukuru Mungu kwa kulifanikisha hili,” alisema.
Aprili
mwaka huu Siwema alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa kosa la kutoa vitisho
kwa kutumia mtandao.
Siwema
na Nay walikuwa ni wapenzi wa muda mrefu ambapo walifanikiwa kupata
mtoto mmoja lakini akiwa bado mchanga, Nay alimfumania mzazi mwenzake
huyo na mwanaume mwingine na hivyo kuvunja uhusiano wao huku akimchukua
mwanaye huyo ambaye kwa sasa analelewa na mama wa Nay.
0 comments:
Post a Comment