Posted by Williammalecela.com on Thursday, June 23, 2016
 |
| Hii ni post ya kwanza ambayo Mange Kimambi alianza kumshambulia nayo Le Mutuz Nation kuhusu mazishi ya Mama yake Le Mutuz aliyefariki Jumamosi iliyopita na kuzikwa Jumatatu na Le Mutuz Nation mwenyewe akishirikiana na na wananchi wa Tunduma alikokuwa akiishi Marehemu Mama yake. Siku moja baada ya mazishi Mange Kimambi ambaye kwa muda wa Wiki Tatu zilizopita amekuwa akishirkiana sana na Mke wa zamani wa Le Mutuz kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii, alizuka kwenye Instagram yake akitumia picha hiyo juu kumdhihaki Le Mutuz kuhusu maisha ya Marehemu Mama yake na kwamba Marehemu alizikwa kama hiyo picha inavyo onyesha. This Blog tuliripoti kama ilivyo bila kupunguza wala kuongeza. |
 |
| Muda mchache baadaye Instagram ililipuka moto baada ya Wananchi wengi waliokasirishwa na uongo wa Mange Kimambi walipokwenda kwenye Kaburi la Mama yake Mange na kupost hizi picha na maelezo makali kwamba Mange anatoa wapi ujasiri wa kutukana Marehemu wa mama wa mwenziwe na huku hata mama yake amelala mahali pabaya zaidi. Hizi ni moja ya Post zilizobandikwa huko Instagram zikionyesha picha ya Marehemu Mama yake Mange na Kaburi lake ambalo lipo kwenye Makaburi ya Waisilamu Temeke. Kufuatia vita hivi Mange alikurupuka tena na kuanza kumshambulia sana Le Mutuz ambaye alirejea jana jioni kutoka Mbeya kumzika Mama yake na ambaye juhudi zote za kumpata kuongea na Blogu hii hazikuwezekana kwa sababu ya kuzimwa kwa simu yake. Bado Blogu hii inaendelea kumstafuta kutaka kujua ana nini la kusema kuhusu mashambulizi haya kwa Marehemu Mama yake. |
0 comments:
Post a Comment