Sunday, June 5, 2016

Meek-Mill-Debuts-Two-New-Songs-on-Hip-Hop-Chart-FDRMX
Rapper kutoka nchini Marekani, Meek Mill ameongezewa kifungo cha ndani cha siku nane baada ya kukiuka masharti ya kifungo cha ndani alichopewa awali cha siku 90 baada ya kukutwa na silaha bila kibali na madawa ya kulevya.

Awali rapper huyo alipewa adhabu hiyo ya kifungo cha siku 90 ndani iliyoambatana na adhabu ya kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea baadhi ya shule kusaidia jamii zinazoishi kwenye maeneo yenye matatizo ya maji.
Aidha alitakiwa kutoa hotuba za uhamasishaji mbele ya umma ambazo mahakama haikuridhishwa nazo kutokana na Meek Mill kuchelewa kufika kwenye baadhi ya vituo tofauti na muda aliopangiwa.
Kifungo hicho cha Meek Mill kitamalizika Juni 9 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment