anawake wanaochelewa kuzaa
wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu
bali maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya. Athari za kuchelewa huko
ni pamoja na
kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti
pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.
Wanawake wengi wanaofanya kazi
huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofika umri a miaka 35 badala ya
kuzaa wakiwa na umri wa miaka 24-28.Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya
afya ya uzazi.
Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini
Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema
kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako
madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari
kubwa.''
Bwana Ong'ech alisema kuwa
wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na
hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.Fibroids zinasababishwa na
kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa
mda mrefu.
Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa
na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .Hatari hizi ni nyingi tu,
sasa chaguo ni kwako.

0 comments:
Post a Comment