Drama
za mastaa wa bongo movies hazeshi (no typo). Jacqueline Wolper na Salma
Jabu maarufu kama Nisha wamepishana lugha huku Harmonize akiwa chanzo.
Issue ilianza vingine kabisa. Nisha alipost picha inayowaonesha Ben Pol, Raymond, Nuh Mziwanda na Rich Mavoko na kuandika: Mmoja
kati ya hawa amejaa kwenye galary ya simu yangu na moyoni mwangu,otea A
B C AU D? enhe. he sa hv siweki hadharani maana nna phd ya kunyakuliwa,
sa hivi ni kumpost kwa mwendo kasiii yaani wengi wengi simtaji ng’ooo.
Watu
walicheka, walifurahi na kucomment hadi pale comment ya mwana bongo
movie mwenzake, Jacqueline Wolper ilipobadilisha kabisa hali ya hewa.
Nisha
alilazimika kuitolea ufafanuzi comment ya Wolper na ndipo mambo
yaliyopo nyuma ya pazia yakawekwa hadharani. Seems like Nisha aliandaa
show Mtwara na kumchukua Harmonize hali iliyomfanya Wolper naye aende
Mtwara – of course kulinda chake kisijekupokonywa!
“Ok
guys kuna picture niliweka saa 4 asbh leo,za wasanii kadhaa wa music
ambao niliweka na caption yangu kwa furaha zangu tu,” aliandika Nisha
kwenye post nyingine.
“Ila
baada ya lisaa limoja ikaja coment hiyo ya msanii mwenzangu
sikudhungumza chchte,i was like ok nikacheka tu. Then zikaja comments
nyingi za kumuuliza kulikoni kuandika hivyo. Masaa mawili yaliyopita
ukaandikwa waraka mzito mrefu unaosema. “Nisha aandaa show Mtwara ya
kumnasa Harmonize ila Wolper akagundua hilo akaamua kuongozana naye
Harmo hadi huko kukwepa hilo (NA MANENO MENGI YA ZIADA YA UONGO.”
“Ikimbukwe
show imeshapita km week na haya maneno yamezuka leo baada ya hiyo
comment. Guyz tuje kwenye point KWANZA KABISA SIJAMLENGA YYTE KWA
NILIYEANDIKA NILIANDIKA KWA MAPENZI YNG KM NILIVYOANDIKA JANA STATUS YA
VIDONDA VYA TUMBO,TENA HADI WADOGO ZNG NIKAWAAMBIA TAZAMA NACHEZA NA
AKILI ZA WATU. NIMESHANGAA HABARI ZA UONGO KUSAMBAZWA ZIDI YANGU TENA
BAADA YA COMENT HII KWANGU,” aliongeza.
“POINT
YA PILI KWA YYTE ANAYEULIZA NIMEANZA LINI UPROMOTA guyz mimi ni
mfanyabiashara na kwenye pesa nipo,show ya MTWARA imenigharimu si chini
ya ml.18 unadhani naweza poteza pesa zote hizo kisa mapenzi?sina ujinga
huo wa akili. NA SIJAWAHI KUMTAKA NA SITOTARAJI KWANZA SIJAZOEA KUPITA
ANAPOPITA MTU HASWA NNAYEMJUA.”
“TATU
nimeandaa show ingine ramadhan ya 13 DAR-ES-SALAAM inahusu ramadhan,
nna SHOW SKUKUU YA IDD MOSS NA IDD PILI MIKOANI ZOTE MM NDO MUANDAAJI NA
KUNA WASANII WAKUBWA TU JE HAO PIA NATAKA KUWANASA? HE. IFIKE HATUA
TUSIWE TUNABALANCE MTU MMOJA NA PIA SIO KILA ASIYEDHUNGUMZA NI MNYONGE
SANA ILA KUNA WKT DRAMA HAZINA MUDA INABIDI UPIGE KAZI MAANA MAISHA
YANAENDA MBELE HAYARUDI NYUMA. NB:SHUKRAN KWA WEWE UNAYESAMBAZA UJUMBE
HUU WA UONGO SINA CHA KUKWAMBIA NIMEPITIA MENGI MAKUBWA SO HILI KM
NACHEZA MDAKO. (mwenye uelewa kaelewa chanzo cha story inayosambaa
imetoka wapi,nimeandika hapa kwa manufaa ya mashabiki zangu wote
watakaobahatika kusoma habari hizo za uongo.”
Na
sasa hebu turejee kwenye post ya mwanzo kabisa ya Nisha. Ni msanii gani
kati yao hao wanne ambaye yupo moyo mwake kwa mujibu wa maneno yake
mwenyewe? Tuanze kudadafua:
BEN POL
Hapana,
juzi tu ametoka kuwa baba na mwanae anaitwa Mali aliyezaa na mchumba
wake wa muda sasa Latifa Mohamed. Jamaa ni mwaminifu.
NUH MZIWANDA
Hapana, juzi tu ameanza kumuonesha mpenzi wake ambaye tayari amejichora tattoo yake. Sio rahisi!
RICH MAVOKO
Hapana, juzi tu mwanae amefikisha siku 40 na kumtoa nje kwa mara ya kwanza na Diamond alikuwepo. Ni ngumu.
RAYMOND
Ewalaaah.. tunaweza kumfikiria hitmaker huyu wa Kwetu kwasababu hadi sasa hajamweka hadharani mpenzi wake.
Ifahamika tu kama alivyosema Nay wa Mitego.
0 comments:
Post a Comment