Glasgow,Scotland.
MAHAKAMA
ya Glasgow’s Justice of the Peace Court ,ya Scotland imetoa hati kwa
wanausalama wa nchi hiyo kumkamata na kumfikisha mahakamani hapo kinda
wa Chelsea ya England,Islam Feruz,kujibu mashitaka matatu yanayomkabili.
Hati
hiyo imetolewa na muendesha mashitaka wa mahakama hiyo Frances
McCartney baada ya Ferouz,20, kushindwa kufika mahakamani hapo wakati
kesi yake iliipoanza kusikilizwa jana Jumatano Juni 8,2016 kwa kile
kinachodaiwa kuwa nyota huyo mwenye asili ya Somalia yuko nchini
Tanzania akifanya mazoezi.
Ferouz
anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kuendesha gari lake la kifahari
aina ya Porsche lenye thamani ya £80,000 wakati akijua fika kuwa
amezuiwa.
Kosa
la pili aliwadanganya maafisa wa polisi waliomkamata kwa kuwaambia kuwa
anaitwa Saeed Cabadalla.Kosa la tatu ni kuendesha gari bila ya kuwa na
leseni.
Ferouz alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Celtic ya Scotland.
0 comments:
Post a Comment