Thursday, June 23, 2016

    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameupongeza mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa jitihada za kutaka kuzifikia kila kaya kwani kufanya hivyo utasaidia wananchi walio katika sekta binafsi na sekta rasmi
Hayo ameyasema leo wakati anafungua mkutano Mkuu wa saba wa GEPF unaofanyika jijini Mbeya ambako mifuko yote ya hifadhi ya jamii ni wanachama wa mfuko huu
Aidha amezindua skimu mpya ya bodaboda ambayo imejumuisha watu wa bajaji na dalaldala ambao kwa kujiunga na kuchangia mfuko huu wanaweza kupata mikopo nafuu na kuweza kumiliki bodaboda kupitia mpango wa bodaboda bila jasho( BBJ)
Amewataka watanzania kote nchini kujiunga na GEOF kwani kila mtanzania ni mstaafu mtarajiwa
  

0 comments:

Post a Comment