Kuna Wakati Nakaa Chini Na Kufikiria Cha Kukulipa Mama Nashindwa Kupata Jibu Sahihi, Nafikiria Nikufanyie Nini Ili Kurudisha Zile Fadhila Zote Lakini Kila Nachokifikiria Naona Hakitoshi Kwako. Nafikiria Shida Na Tabu Ulizopata Kuniweka Tumboni Mwako Kwa Miezi 9, Kuna Muda Hukulala Na Kuna Muda Ulihangaika Kwenda Na Kurudi Hospitali Ili Tu Niweze Kufikisha Muda Na Kutoka Tumboni Kwako Nikiwa Salama. Nafikiria Kipindi Cha Uchungu Wa Uzazi Na Hata Baada Ya Kunizaa Ukaendelea Kunilea Na Kuacha Starehe Zako Na Raha Zako Zote Ili Uhakikishe Ninakua Kwenye Maadili Mema Na Nikiwa Na Afya Njema. Kuna Muda Ulifikia Hata Kugombana Na Ndugu Na Majirani Mradi Tu Unitetee Na Nisijione Mpweke, Ulijinyima Hata Kuvaa Vizuri Ili Univalishe Mie Kipindi Cha Sikukuu Nisijione Tofauti Na Watoto Wengine. Ulinisomesha Kwa Juhudi Zako Zote Na Hukuacha Kunipa Ushauri Pale Ulipoona Ninakwenda Nje Ya Mstari Na Kuna Wakati Nilikukosea Lakini Hukunitupa Ukijua Ni Ujana Tu Utapita. Na Hata Sasa Nimekuwa Mtu Mzima Lakini Bado Hujaniacha Na Unanipenda Kama Mwanzo Na Ndo Kwanza Mapenzi Yako Kwangu Yanaongezeka. Wewe Ni Zaidi Ya Mama Kwangu, Wewe Ni Rafiki, Wewe Ni Mungu Wangu Wa Pili Hapa Duniani, Uwepo Wako Kwangu Ni Furaha Tosha, Hata Dunia Ikinigeuka Nikikufikiria Wewe Napata Nguvu Ya Kusonga Mbele. Ahsante Sana Mama! @mama_mobetto @mama_mobetto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment