Tuesday, June 7, 2016

11386515_256216594739694_825283239_n
Baada ya siku chache kuongezewa kifungo cha siku nane ndani ya nyumba yake, rapper Meek Mill amevunja sheria hiyo kwa kutoka nje.

Meek Mill alienda pamoja na mpenzi wake Nick Minaj kwenye tamasha la Queen Bey ‘Formation Tour’ huko Philadelphia na alipanda jukwaani na kuimba wimbo pamoja na Dj Khaled na Rick Ross.
Meek Mill aliongezewa kifungo hicho cha siku nane ndani ya nyumba yake kutokana na mahakama kutoridhishwa na utendaji kazi wa rapper huyo aliopewa kama adhabu na mahakama.
Hata hivyo inadaiwa kuwa alipata ruhusa kutoka kwa jaji kuhudhuria kwenye tamasha hilo.

0 comments:

Post a Comment