Thursday, June 23, 2016

Nuh akiwa na mpenzi wake mpya aitwae Nawal
Katika hali inayoonekana siyo ya kawaida, mapenzi yanamfanya Nuh Mziwanda apingane na kauli zake mwenyewe alizowahi kusema.

Nuh Mziwanda ni mmoja kati ya wasanii wachache wa muziki wa Bongo Fleva waliobarikiwa kipaji kikubwa cha kuimba japo kuwa nyota yake imeonekana kufichwa na mwanga wa jua la mchana linalowaka lakini likiingia giza hapo ndipo mwanga wa nyota yake utakapoonekana.
Mwezi Mei mwaka huu akiongea kwenye kipindi cha 5 Selekt, kinachoruka kupitia EATV, Nuh Mziwanda alisema, “Kwa sasa sitaki tena maisha ya skendo na kiki ndiyo maana hata kwenye page yangu mpya huoni watu wakimtukana Nuh tofauti na ilivyokuwa zamani.”
Kauli hiyo inaonekana kupingana na ukweli uliopo kuwa, ukiangalia akaunti ya Nuh kwa sasa utaona picha nyingi akiwa na mpenzi wake, Nawal zikiwa zimeambatana na maonyesho ya tattoo mpya walizozichora na kutukumbushia maisha ya mwanzo ambayo Shilole aliwahi kufanya wakati wapo kwenye mahusiano na Nuh.
NNNN
Akiongea na Global mwezi Octoba mwaka jana, Shilole aliwahi kusema, “Mimi bado tattoo moja ya muhimu sana ambayo nataka kuchora kwenye kalio ili kuonyesha ni jinsi gani nampenda mpenzi wangu Nuh,” lakini mwisho tuliona kilichotokea.
Ni kweli wimbo wa ‘Jike Shupa’ umemweka Nuh kwenye ramani nzuri ya muziki Bongo na kurudisha heshima yake iliyopotea kwa muda mrefu ya kuonekana ni kama msanii wa kawaida tu, lakini kitu anachopaswa kukitambua ni kusimamia muziki wake na kutosahau ile kauli inayosema ‘mtu aking’atwa na nyoka, akiguswa na jani anaruka.’

0 comments:

Post a Comment