Friday, June 3, 2016

CkBxt_LW0AAsFXz
Vanessa Mdee Ijumaa hii aliiwakilisha taasisi ya One Campaign kuwasilisha sahihi 150,000 za kampeni ya #StandWithEva bungeni mjini Dodoma.

Huko alikutana na waziri mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine pamoja na Eve mwenyewe
CkByvLeXEAAgZZc
Binti Eva kwenye t-shirt ya Blue akiwa na wanafunzi wenzake pamoja waziri mkuu, Vanessa na viongozi wengine bungeni
CkBaewaXEAAmH5P
Ni binti kutoka Iringa. Eva anataka maisha bora kwa familia yake na kwake. Anaamini anaweza kufikia lengo lake kwa kupata elimu nzuri. Hata hivyo Eva ana changamoto kubwa. Kijiji chake cha Malinzanga kina upungufu mkubwa wa maji. Muda anaotakiwa kuutumia shuleni anautumia kuchota maji na kufanya kazi nyingine za nyumbani.
13269544_250107978691923_394519542_n
Vanessa akiwa na Eva

Eva alituma maombi kupata msaada toka serikali ya kijiji lakini hakufanikiwa. Binti huyu hakukata tamaa. Alimuandikia Barack Obama #POTUS barua. Ombi lake lilisikika na #POTUS wakampa nafasi wakati wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa. Baadaye #StandWithEva ilitengenezwa na One Campaign na Restless Development. Baada ya sahihi 150,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
CkBQQq3WEAEVnpY
13320067_618498804975181_1207839049_n

0 comments:

Post a Comment