MWANAMUZIKI
mwenye jina kubwa Afrika, 2 Face Idebia amempa shavu la mwaliko diva
anayekimbiza kwenye Tasnia ya Muziki Bongo, Vanessa Mdee ‘V Money’
kwenye tamasha lake litakalofanyika leo jijini Nairobi, Kenya huku
wasanii mbalimbali kutoka kila kona ya Afrika wakitarajia kufanya
makamuziki ya ukweli.
Akizungumza na gazeti hili, V-Money anayetamba
na Wimbo wa Niroge kwa sasa amesema shavu hilo kwake ni kitu kizuri
maana kimeonesha ni jinsi gani wasanii wa nje wanavyothamini kazi zake
hata kuamua kumpa mwaliko ambao mbali na kutangaza ngoma yake ya Niroge
atapata fursa ya kukutana na wasanii wengi ambao anaweza kupata wa
kufanya nao kazi.
“Namshukuru Mungu kazi zangu zinaheshimika, mwaliko
wa 2 Face ni muhimu kwangu na nimeuchukulia kwa uzito kutokana na
tamasha lenyewe litakavyokuwa kubwa, nina uhakika sitaondoka bure,
lazima nitapata lolote la kufanya kwa mashabiki wangu,” alisema V-
Money.

0 comments:
Post a Comment