DAR
ES SALAAM: Bado habari ni moto! Majonzi yanaendelea kutawala kwenye
familia ya Bilionea Erasto Msuya (43) aliyeuawa kwa kupigwa risasi
Agosti 8, 2013, Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia)
kufuatia safari hii, mdogo wake wa kike, Aneth Simon Msuya (30) naye
kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Uwazi limebaini
mchezo mzima.

Aneth
(pichani) alifanyiwa ukatili huo, Mei 26, mwaka huu chumbani, nyumbani
kwake, Block 16, Kibada- Kigamboni jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto
wake, Allan Kimario.
Mauaji
hayo yaligunduliwa na jirani asubuhi baada ya mtoto wa marehemu, Allan
kwenda kusema mama yake haamki na yeye anataka kwenda shule huku basi la
shule likiwa limemwacha. Pia alisema anahisi njaa.
Jirani
huyo aliongozana na mtoto huyo hadi ndani na kuubaini mwili huo ukiwa
umalala sakafuni kwenye dimbwi la damu na kisu kilichotumika kumchinjia
kikiwa pembeni yake na hivyo kutoa taarifa polisi.
Tangu
kutokea kwa tukio hilo, vyombo mbalimbali vya habari nchini vimekuwa
vikiripoti tukio hilo katika njia za kusikitisha sana kutokana na unyama
aliofanyiwa Aneth na ndipo, Uwazi nalo likazama mitaani kuchimba kwa
kina ili kuwapa wasomaji wake mambo mapya zaidi.
Madai
yaliyosambaa ni kwamba, kuna kundi la watu limepanga mkakati mzito wa
kuhakikisha familia ya Msuya inafutika kwenye uso wa dunia kutokana na
kisasi cha kibiashara (bila kufafanuliwa).
“Ilivyo
ni kwamba, baada ya kaka yao (Erasto) kuuawa, kwa kupigwa risasi, kuna
kundi la watu limeamua kuifuta familia hiyo kwenye uso wa dunia. Ndiyo
maana mbali na Aneth kuchinjwa, kuna akina Msuya wengine wameshakumbana
na vitendo vya kuashiria kwamba, roho zao zinasakwa
Kwa
mujibu wa chanzo kimoja toka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania,
msichana anayedaiwa kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’ nyumbani kwa
marehemu Aneth na kuondoka siku ya mauaji hayo, anapewa nafasi ya kwanza
katika kuchunguzwa akisemekena kuujua mchezo mzima wa kifo cha bosi
wake huyo na sasa jeshi hilo linamsaka kwa udi na uvumba.
“Kwanza
nataka kusema kuwa, hausigeli ndiye mshukiwa wetu wa kwanza ndani ya
jeshi la polisi. Huyu msichana wa kazi aliondoka mchana, usiku yakatokea
yaliyotokea, akipigiwa simu hapatikani.
“Huyu
tunamtuhumu kuujua mchezo wote. Kwa hiyo pa kuanzia kwetu tunafanya juu
chini kumpata ili aisaidie polisi,” kilisema chanzo hicho huku kikiomba
hifadhi ya jina kwa vile, si msemaji sahihi wa jeshi hilo.
ALIPANDIKIZWA?
Pia,
chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, utafiti wa awali wa jeshi hilo
unataka kukubaliana kwamba, kutokana na mlolongo unaotokea wa mauaji au
kujeruhiwa kwa watu mbalimbali wa familia ya Msuya, kuna uwezekano
msichana huyo wa kazi alipandikizwa na watu hao kufanya kazi kwa Aneth.
“Kuna
wasiwasi yule dada wa kazi alipandikizwa. Kuna uwezekano alifika pale
katika njia za mtego ili kumsoma Aneth na mazingira yake pamoja na
mwenendo, sasa baada ya kukamilisha ndiyo akaamua kuondoka na usiku
wauaji wakafika. Kwa hiyo hayo yote sisi polisi tunayachunguza,”
kilisema chanzo.
WAUAJI WALIINGIAJE NDANI?
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, inaaminika kwamba, wauaji hao walifanikiwa
kuzipata funguo halisi za geti kubwa la mlango wa kuingilia sebuleni kwa
Aneth, wakaenda kuchongea nyingine ambazo siku walipofika, waliweza
kufungua geti na kuingia kama kwao.
“Lile
geti kubwa linafunga kwa nje na funguo, kwa ndani unavuta loki tu. Kwa
hiyo wao waliingia ndani kwa kufungua. Walipomaliza kutenda ukatili wao,
inaonekana walifunga geti kubwa kwa kuloki ambapo kwa mtu mwingine wa
nje asingeweza kuingia ila yule mtoto (Allan) aliweza kutoka nje kwa
sababu loki yake ni ya kubetua tu.”
KWA NINI WAUAJI WALIIBA TIVII TU?
Chanzo
hicho kikasema kuwa, watuhumiwa hao hawakuiba kitu zaidi ya tivii
(flat) lakini inaonekana kwamba waliamua kuichukua runinga hiyo kwa vile
waliamini ni skrini kwa ajili ya kamera za ulinzi (Closed-Circuit
Television au CCTV) ambapo walijua picha zao zilichukuliwa. Hata hivyo,
tivii hiyo waliitupa mbele ya safari.
HAIKUWA RAHISI KUMCHINJA ANETH
Chanzo
hicho kilisema kuwa, mazingira ya chumba yalionesha kuwa, kabla ya
kuchinjwa, kulikuwa na purukushani kubwa kwani neti ilikutwa imechanwa,
baadhi ya vitu vimepinduliwa, vingine vimezagaa kila mahali hali ambayo
iliashiria kuwa, marehemu hakukubali kuchinjwa kirahisi.
MAISHA YA ANETH
Baadhi
ya watu waliozungumza na gazeti hili wakidai kumjua dada huyo, walisema
kuwa, baada ya kifo hicho wamebadili mawazo kuhusu yeye kuwa huenda
alijua anawindwa.
“Awali
tulijua ni dada anayeringa, kwani alikuwa akifika dukani, anaegesha
gari jirani kabisa na mlango wa duka kisha anaagiza kitu anachokitaka,
anapelekewa, analipa pesa anaondoka.
“Hata
siku tatu kabla ya kifo, alifika kwenye kibanda cha chipsi, akaagiza na
kufungiwa akiwa ndani ya gari. Alikuwa hana kawaida ya kushuka, huenda
alijua anawindwa,” alisema mkazi mmoja wa maeneo ya Kibada huku akiomba
hifadhi ya jina lake.
SIMU ZA KUULIZWA ALIPO
Mmoja
wa watu waliodai kufanya kazi na marehemu wizara ya fedha, alisema
kuwa, wiki chache nyuma, Aneth aliwahi kusema kuwa, kuna wanaume
wamekuwa wakimpigia simu na kumuuliza; Aneth uko wapi?’ lakini akiuliza
we nani? Simu inakatwa!
“Huenda
wale watu nao si sehemu ya watuhumiwa hawa. Maana hali hiyo alisema
hakuwahi kukumbana nayo siku za nyuma. Baada ya kusikia amechinjwa sasa
nahisi huenda Aneth alifuatiliwa kwa siku nyingi nyuma lakini yeye
alikuwa hajui,” mtu mmoja aliliambia Uwazi kwa kumkariri mfanyakazi
mmoja wa wizara hiyo.
MAISHA YAKE NA MAJIRANI
Baadhi
ya majirani na nyumba ya marehemu walisema kuwa, haikuwa rahisi kubaini
mienendo ya watu wasioeleweka nyumbani kwa Aneth kwa vile maisha yake
yalikuwa hayasomeki kwa mwanga wa kawaida.
“Alikuwa
akikuona anakusalimia akiwa ndani ya gari, akiingia kwake ameingia.
Sasa isingekuwa rahisi kumjua kwa undani yeye na wageni wanaofika kwake.
Lakini mimi nimewahi kusikia kwamba, Aneth aliolewa ila kwa bahati
mbaya ndoa yake ilivunjika mwaka mmoja na baba wa mtoto wake,” alisema
jirani mmoja kauli ambayo pia ilithibitishwa na dada mmoja wa Aneth.
NDUGU WASHTUKA, WAWEKA MLINZI
Gazeti
la Uwazi pia lilifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu ambapo lilikuta
nyumba inalindwa na mlinzi ambaye alisema aliwekwa hapo baada ya mauaji
hayo.
UWAZI OFISINI KWA RPC TEMEKE
Hayo
yote yalikuwa maneno mbalimbali ya vyanzo vyetu, hivyo mwishoni mwa
wiki iliyopita, Uwazi lilifika ofisini kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke, ACP Gilles Mroto ili kumsikia kama ana mtiririko huo, lakini kwa
upande wake, alisema kuwa, wapo katika msako mkali kuwasaka wauaji hao.
“Hata
huyo hausigeli pia tunamsaka sana ili kulisaidia jeshi la polisi kwa
vile uondokaji wake na mauaji kuna utata,” alisema Kamanda Mroto.
MATUKIO YA KUIANDAMA FAMILIA
Tangu kutokea kwa mauaji ya Erasto, kumekuwa na matukio mengi ya kuiandama familia hiyo kwa kutaka kuwatoa roho wahusika.
KUNA ALIYEMWAGIWA SUMU
Dada
wa Aneth aliyetajwa kwa jina la Antuja aliwahi kumwagiwa kitu
kinachosadikiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na mtoto wa
Aneth, Allan hivyo kuathirika na sumu hiyo.
TUKIO LA HONGERA BAR
Desemba
mwaka jana, dada mwingine aitwaye Ester na muwewe walipigwa risasi
mgongoni na kifuani wakiwa katika Baa ya Hongera, Kijitonyama, Dar.
Mwili wa Aneth alisafirishwa jana kwenda Kijiji cha Kairo, Mererani, Simanjiro, Manyara kwa mazishi. Mungu aiweke pema peponi, roho yake. Amina.
0 comments:
Post a Comment