Kama mzaha vile, bila kujali ukubwa wa
kiingilio, Chirstian Bella anaujaza ukumbi mkubwa wa Escape One katika onyesho
lake maalum la miaka yake 10 katika ‘game’ hapa Tanzania.
Escape One ikashona watu mithili ya njiti
za kibiri zinavyobanana kwenye box lake huku burudani za nguvu zikishushwa bila
kikomo.
Katika mambo yaliyovutia ni pamoja na
Bella kumwalika bosi wake wa zamani aliyemleta hapa Bongo - Prof. Juma Kapuya
(mmiliki wa Akudo Impact.
Kapuya akawa ni mmoja wa watu muhimu
waliolishwa keki na Christian Bella.
Kiingilio cha onyesho hilo kilikuwa ni elfu 20 na elfu 50 kwa ma-VIP.
Christian Bella ameandika historia mpya katika maonyesho yake
Christian Bella akimlisha keki Prof Juma Kapuya
Dully Sykes (kushoto) na Khamis Dacota wa Clouds TV wakifuatilia onyesho la Bella
Source:- Saluti







0 comments:
Post a Comment