STAA
wa filamu Bongo, Chuchu Hans anadaiwa kunasa ujauzito wa mchumba wake
ambaye naye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’. Kwa mujibu wa
chanzo ambacho kipo karibu na wawili hao, Chuchu kwa sasa ni mtu wa
kujifungia ndani na amekuwa hapatikani kwenye matukio mbalimbali
yanayomhusu. “Ameshanasa, tena ujauzito huo ni wa Ray, unaambiwa sasa
hivi kawa mtu wa kujifungia ndani tu na kitumbo kimeshamtoka,” kilisema
chanzo.
Alipotafutwa
Chuchu kujua ukweli alijibu; “Nashangaa, watu wengi wananifikiria hivyo
lakini sitaki kuongea chochote. Labda watakuwa na husda tu ndiyo maana
wananifikiria hivi,” alisema Chuchu. Ray alipotafutwa kwa njia ya simu
ili kusikia kauli yake hakupokea
0 comments:
Post a Comment