‘Kinda’
wa Bongo Fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ ambaye anatamba na kibao
chake cha Bado, anadaiwa kumnunulia mpenzi wake, staa wa filamu,
Jacqueline Walper ‘Wolper’ gauni lenye thamani ya shilingi milioni moja, Risasi Jumamosilimetonywa.
Chanzo
kilicho karibu na msanii huyo wa lebo ya WCB, kinadai muigizaji huyo ni
mwanamke wa gharama, ambaye mavazi na maisha yake, yanahitaji mtu
mwenye uwezo kifedha, lakini kwa kijana huyo mwenyeji wa Mtwara ni kama
anajiumiza.
“Yaani
hivi karibuni wakati akienda kumtambulisha kwao, alilazimika kumnunulia
gauni la shilingi milioni moja wakati yeye mwenyewe anavaa mavazi ya
kawaida tu kama wasanii wenzake, hapa kweli mapenzi yamekubali,”
kilisema chanzo hicho, kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Wolper na kumsomea
tuhuma hizo, lakini alicheka na kudai hana la kusema kwa vile maisha ya
kimapenzi na msanii huyo ni ya kawaida tu.
Harmonize
mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema kwa wakati huo
hakuwa katika eneo zuri, akiahidi kupiga yeye mwenyewe kwa gazeti hili
baadaye lakini hadi linakwenda mitamboni, hakuwa amepiga.
Kwa upande wa meneja wa msanii huyo, Mohamed Salum ‘Rikadomomo’ alisema anamsimamia kimuziki tu, maisha yake binafsi hayamhusu.
0 comments:
Post a Comment