Ikiwa
ni siku chache toka Ex wa Shilole, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo
‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake huyo,
Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.Nuh
amethibitisha kwamba Shilole ndiye aliyemuimbia kwenye wimbo huo, kwa
kumtumia video queen anayefanana na Shilole kama pacha katika video ya
wimbo huo.
Sholole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe instagram ambao baadae aliutoa:
"Wale
unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani
kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote
mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza
kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitengo. Umemiss mkong’oto?.
Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha…
Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako.
Nikifungua mdomo wangu utadhalilika....." Shilole
Shilole
na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa
alizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na
mwanadada huyo, huku Shilole akitaa kuzungumzia kilichotokea.

0 comments:
Post a Comment