Stori: Gladness Mallya
STAA
wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi ambaye alipata kiki ya aina yake
kwa kibao chake cha Majanga, amefunguka kuwa licha ya kupata shoo
nyingi kupitia ngoma hiyo, lakini pia alipata majanga kwa kutapeliwa
mara kadhaa.
Akipiga
stori na Risasi Vibes, Snura alisema promota mmoja alimpeleka kufanya
shoo mkoani Kilimanjaro na Mererani Arusha, lakini baada ya kuwa
ameshafanya kazi, mtu huyo alimkimbia bila kumpa chake, kiasi kwamba
alilazimika kurejea Dar kwa lifti.
“Sitasahau,
nilisaidiwa lifti mimi na wacheza shoo wangu kutuleta Dar, lakini
baadaye nilikuja kumpata huyo promota, nikamnyang’anya pete ya ndoa na
uchumba, ninazo mpaka leo maana hakunilipa,” alisema Snura.
0 comments:
Post a Comment