Ni miezi kadhaa sasa tangu video ya ‘chura’ kufungiwa na serikali hadi itakaporekebishwa, Snura amewasilisha script bodi ya filamu kwa ajili ya kuifanyia video nyingine, AYO TV imetaka kujua maamuzi ya bodi ya filamu baada ya script ya snura kufikishwa kwenye bodi. Akizungumza na Ayo TV mtendaji wa Bodi ya filamu nchiniJoyce Fissoo amesema
>>>”Snura aliwasilisha script ndogo kwa ajili ya kuitengeneza tena, hata hii aliyoileta bado ilikuwa na muelekeo huo, haikuwa na tofauti na ile ya mwanzo, haikuwa na maudhui na haikufafanua hasa anataka kupeleka ujumbe gani kwa jamii’
>>>’kamati haijaridhia ile script yake kwenda kutengenezea video, mhusika anayo haki ndani ya siku 30 toka maamuzi yametolewa kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana lakini jana tumepokea barua ameleta script nyingine amesema amefanyia marekebiso bado tunaifanyia kazi’
0 comments:
Post a Comment