Mmoja kati ya mameneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kuwa msanii wake yupo booked mpaka mwezi August mwaka huu.
Akizungumza na Swahili Talk Radio, Sallam alisema yeye na mameneja wenzake wamehakikisha msanii wao anapata show za kutosha.
“Kila mwaka unapoanza lazima tuwe na ajenda ya kutengeneza program ya mwaka mzima, ndio maana mpaka sasa unakuta show zimeanza February na tupo booked mpaka mwezi August,” alisema.
“Kama mimi sasa hivi nafanya maandalizi ya tour yetu ya Marekani na mambo yanaenda poa. Kwa sababu watu wengi walikuwa wanahofu asije akatangazwa anakuja halafu asije ndio maana mimi nipo huku kuweka mambo sawa,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment