Friday, June 10, 2016

um1
Awali ya yote, napenda kuwashukuru kwa kujumuika nasi ili niweze kuongea na wananchi kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani.

Kila mwaka tarehe 14 Juni, dunia inaadhimisha Siku ya Wachangia Damu  Lengo la maadhimisho haya ni kukuza uelewa kuhusu huduma ya damu salama, kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari na pamoja na kuwatambua na kuwaenzi watu ambao wamekuwa wakichangia damu kwa hiari kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu.
Aidha, Siku ya Wachangia Damu Duniani ni ukumbusho wa siku ya kuzaliwa ya Ndugu Karl Landsteiner, ambaye ndiye aliyegundua mfumo wa makundi ya damu ya “A”,”B” na “O”, na alizawadiwa tuzo ya Nobel kutokana na ugunduzi huo.

Mwaka huu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama inatarajia kuadhimisha Siku ya Wachangia Damu Duniani kwa kuhusisha Mikoa yote ambayo pia itashiriki katika kampeni ya Siku ya Wachangia Damu Duniani kwa kukusanya damu kila Mkoa, angalau Chupa za damu 100 kwa kila Halmashauri, Lengo ni kukusanya chupa 20,000 nchi nzima.
Kitaifa Maadhimisho haya yatafanyika tarehe 14/6/2016 hapa Mkoani Dodoma kwa kuhusisha vyuo vikuu vilivyopo Mkoani Dodoma, ambapo vitashiriki katika zoezi la kuchangia damu. Aidha, kilele cha maadhimisho hayo kitatanguliwa na kampeni ya siku mbili ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari na ukusanyaji wa damu. Ili kuendana na kauli mbiu ya ‘’HAPA KAZI TU” hakutakuwa na sherehe au shamrashamra zozote zaidi ya kukusanya damu.

0 comments:

Post a Comment