Tasnia
ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya
kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku
moja zikatimia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kama
ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo
pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top
10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya
kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21
lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji
cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia
‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado
anaonekana ni mwenye kuvutia.
Ni
mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa
sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo
kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji
alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa
na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na
mwananamuziki.
Huyu
ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa
kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya
kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
Huyu
ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa
maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula
aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali
inayomfanya autunze urembo alionao.
Ana
umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na
mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume
kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna
anavyouvaa uhusika.
Amezaliwa
miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na
mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba
kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
Huyu
ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri
kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku
zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
Hivi
unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye
tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako
binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike
kwenye filamu nyingi za Nigeria.
Huyu
ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye
mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya
urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa
uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.
Wafuatiliaji
wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40
lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.
0 comments:
Post a Comment